June 26, 2017


NDIKUMANA WA KWANZA KUSHOTO, AKIWA NA KIKOSI CHA MBAO FC.

Uingozi wa klabu ya Mbao FC umethibitisha kiungo wao mkabaji Mrundi, Yusuph Ndikumana kurudi kuichezea timu hiyo baada ya kushindwana na Klabu ya Yanga.

Mrundi huyo, alikuwa akiwaniwa vikali na Simba na Yanga lakini alitangaza dau la shilingi milioni 40 ili asaini mkataba.

Kiungo huyo, ni mchezaji huru hivi sasa anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji kwa mujibu wa kanuni za Fifa kutokana na mkataba wake Mbao kumalizika.

Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi, amesema kiungo huyo atarejea kuichezea timu hiyo baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Yanga.
Njashi alisema, kikubwa kilichokwamisha kiungo asisaini Yanga ni dau la usajili.
Aliongeza kuwa, tayari wamewasiliana na kiungo huyo, na kuanzia wiki ijayo atarejea nchini kwa ajili ya kumalizana na Mbao.
“Kati ya wachezaji wenye mapenzi na moyo wa kuichezea Mbao, basi ni Ndikumana, alikuwa yupo tayari kuendelea Mbao hata kama ingeshuka daraja.
“Hivyo, wiki iliyopita tulifanya naye mawasiliano akiwa nyumbani kwao Burundi na kutuambia kuwa anarejea kuichezea Mbao, hiyo ni baada ya kushindwa kufikia muafaka na Yanga.

“Yanga walionyesha nia kubwa ya kumsajili lakini dau la usajili ndiyo lilikuwa tatizo, hivyo Ndikumana tutabaki naye msimu ujao wa ligi kuu,” alisema Njashi.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic