July 7, 2017


Sahihi kusema Mwenyezi Mungu ni mkubwa na kila nafsi itaonja mauti.

Habari si njema katika familia ya soka ya England na duniani kote, nayo ni kifo cha mtoto Bradley Lowery.

Bradley shabiki namba moja wa Sunderland na rafiki namba moja wa mshambulizi mkongwe wa Sunderland na England, Jermain Defoe.

Mtoto huyo aliyekuwa amefikisha miaka sita alianza kupambana na ugonjwa wa kansa tokea mwaka 2013 na alikuwa maarufu baada ya urafiki wake kusikika kila sehemu. 


Mwenyezi Mungu amrehemu.

1 COMMENTS:

  1. Mungu ktk neno lake hajasema kila nafsi itaonja mauti, hayo ni maneno ya Qur'an sio maandiko mtakatifu.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV