July 8, 2017Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Ajibu amejitapa kuwa ujio wa mshambuliaji, Ibrahim Ajibu kutoka Simba kutazidi kuiongezea makali safu yao ya ushambuliaji.

Yanga wamekata mzizi wa fitina baada ya Jumatano wiki hii kumtambulisha Ajibu kuwa mchezaji wao mpya kwa msimu ujao baada ya kumsainisha kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Simba.

Ajibu anaungana na washambuliaji wengine wa kikosi hicho wakiwemo Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa. 

Akilimali amesema kuwa, anaamini kuongezeka kwa Ajibu katika safu yao ushambuliaji kutazidi kuiongezea makali timu yao kutokana na uwezo mkubwa alionao.

“Ajibu ni miongoni mwa wachezaji wazuri sana, ujio wake tunaamini utaleta mabadiliko katika safu ya ushambuliaji akishirikiana na wachezaji wenzake aliowakuta na wale wanaosajiliwa.


“Ni matumaini yetu sisi kutokana na uwepo wake pamoja na kina Ngoma na Tambwe ile safu yetu ya ushambuliaji itakuwa bora sana msimu ujao na itatisha kuliko msimu huu uliomalizika,” alisema Akilimali.

1 COMMENTS:

  1. Katibu wa baraza la wazee la Yanga Ibrahimu AJIBU???

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV