July 7, 2017


Huku kikosi cha Simba kikianza maandalizi yake ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, juzi Jumatano, kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog anatarajia kutua nchini kesho Jumamosi tayari kwa kuanza kukisuka kikosi hicho.

Katika mazoezi hayo juzi ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Chuo Kukuu Cha Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, hakuna kocha yeyote wa timu hiyo aliyekuwepo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Omog amesema kuwa anatarajia kutua nchini kesho Jumamosi usiku baada ya kukamilika kwa taratibu zote za safari yake hiyo ya kutoka kwao nchini Cameroon ambapo atapitia nchini Kenya na baadaye atakuja Dar es Salaam.

“Nasikia timu imeanza maandalizi jana (juzi) tayari kwa ajili ya msimu ujao ila mimi Mungu akipenda nitafika hapo nchini Jumamosi usiku na Jumatatu nitaanza rasmi kazi.


“Kuhusiana na mambo mengi ikiwa ni pamoja na usajili wa wachezaji ambao umefanyika mpaka sasa, nitazungumzia pindi nitakapofika huko,” alisema Omog.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV