July 1, 2017Wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya TFF, wameonyesha wazi wao wanataka kubadili utaratibu sahihi wa kamati hiyo ili kutoa nafasi wagombea walio mahabusu nao kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi.

Jamal Malinzi anayegombea urais kutetea kiti chake na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ anayewania makamu mwenyekiti wapo mahabusu wakituhumiwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Lakini watu wa kamati hiyo wameonekana kutofautiana baada ya mwenyekiti kusisitiza, kesho ndiyo mwisho wa usaili na ambaye hatatokea kama kanuni zinavyosema zinaeleza atakuwa amejitoa katika uchaguzi.

Wajumbe wameonekana kumpinga mwenyekiti wakitaka ufanyike usajili hata wa kuandika tu.

Maana yake walio mahabusu wanaweza kuandika barua na kujieleza na usaili ukafanyika jambo ambalo linaonekana kupindisha utaratibu.

Awali, mwenyekiti alifanya kikao na waandishi wa habari leo mchana na kusema wazi sahihi ni anayekosa usaili anakuwa amejiondoa.

Alipoondika, wajumbe nao wakafanya mkutano na waandishi. Hawakuonyesha wanampinga mwenyekiti lakini wakasisitiza kuwa usaili unaweza kufanyika kwa maandishi au hata baada ya siku tatu zilizotangazwa za usaili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV