July 1, 2017




Uongozi wa Yanga umekubali kuwa ilibaki kidogo tu watani wao Simba wamtwae straika wao hatari, Donald Ngoma.

Yanga wamesema Ngoma alikuwa anafuatwa na kusumbuliwa na viongozi wa watani wao wa jadi, Simba waliotaka kumsajili kabla ya wao kumuongezea mkataba.

Kauli hiyo, imekuja ikiwa ni siku chache tangu Yanga wafanikiwe kuzima jaribio la Simba kutaka kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe.

Jumatano ya wiki hii, Yanga ilimuongezea mkataba wa miaka miwili Ngoma ambaye sasa atabaki kuichezea timu hiyo kwa misimu miwili ijayo.

Akizungumza katika Kipindi cha Spoti Hausi kilichorushwa na Global Tv Online, juzi Alhamisi, Kaimu Ofisa Habari wa Yanga, Godlisten Chicharito alisema, kabla ya msimu uliopita Ligi Kuu Bara kuisha walipata taarifa za viongozi wa Simba kumsumbua Ngoma kwenye simu.

Chicharito alisema, Simba walikuwa wanamshawishi Ngoma akasaini kwao baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita na kumtaka asiongeze mkataba Yanga.
Alisema wao baada ya kupata taarifa hizo, hawakupoteza muda kushindana na Simba badala yake walizungumza na Ngoma na a naye mambo ya msingi hadi alipoongeza mkataba.

“Mimi ukitoa nafasi yangu ya uongozi niliyokuwa nayo Yanga, ni rafiki wa karibu wa Ngoma na ninakaa naye mtaa mmoja, hivyo vitu vingi tunazungumza.

“Kati ya vitu hivyo ni taarifa za Simba kumpigia simu wakimshawishi kuwa asiongeze mkataba Yanga na badala yake akasaini Simba, hivyo baada ya kupata taarifa hizo tukamuuliza na mwenyewe akakiri.

“Akatuambia bado hajaifanyia makubwa Yanga katika msimu uliopita wa ligi kuu kutokana na kukaa nje muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.

"Hivyo aliomba aongeze mkataba mwingine ili msimu ujao wa ligi aifanye mambo makubwa na ndiyo maana akaachana na Simba na kusaini tena Yanga,” alisema Chicharito.



2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic