July 8, 2017



Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke, amewasili jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwao Mbeya na wakati wowote atamwaga wino kwa ajili ya kuendelea kuichezea timu hiyo.

Hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu taarifa zienee kuhusu kiungo huyo kwenda Singida United inayofundishwa na Hans van Der Pluijm aliyekuwa anaifundisha Yanga.
Kiungo huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayomhitaji kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kaseke amesema amerejea Dar juzi Alhamisi jioni kwa ndege kutoka Mbeya baada ya uongozi kumuita kwa ajili ya mazungumzo.

Kaseke alisema, mara baada ya kutua moja kwa moja alikutana na viongozi kwenye makao makuu ya timu hiyo iliyokuwepo mitaa ya Twiga na Jangwani na kufanya nao mazungumzo.

Alisema mazungumzo yao yamefikia pazuri na uongozi huku akisema anasubiria dau pekee litakalomshawishi yeye kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili.

“Nipo Dar hivi sasa nimekuja leo (juzi) jioni kwa ndege nikitokea nyumbani Mbeya nilipokwenda kwenye mapumziko mafupi baada ya ligi kuu.

“Nimekuja baada ya viongozi wa Yanga kunipigia simu nije Dar kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili.

“Mazungumzo yanaenda vizuri na mambo yakienda sawa, basi nitasaini Yanga japokuwa kuna timu nyingine baadhi za ligi kuu ambazo zinanitaka,” alisema Kaseke.


Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika kuzungumzia hilo alisema: “Nitafute baadaye kidogo, hivi sasa ninaingia kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji cha Yanga.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic