September 19, 2017

KABWILI, KIPA KINDA WA YANGA (KUSHOTO) AKILALAMIKA KWAMBA HATAKI KUPIGWA PICHA, HUKU WACHEZAJI WENGINE WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZAO, HUENDA WALIJUA KINDA HUYO HAJUI ENEO LA WAZI HAUWEZI KUZUIA KUPIGWA PICHA NA HASA KWA WATU MAARUFU KAMA WACHEZAJI. BAADHI YA WACHEZAJI WANAOLIJUA HILO WALIENDELEA NA SHUGHULI ZAO NA BAADAYE WALIMUITA NA KUMPA MAWAZO KUHUSIANA NA HILO.

Kikosi cha Yanga, kimeshindwa kufanya mazoezi leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Pamoja na wachezaji kujitokeza mazoezini, lakini walikusanyika pamoja na kufanya mazungumzo na baada ya hapo kila mtu akachukua hamsini zake.

Kwa waliokuwa mazoezini, hakuna aliyetaka kulizungumzia suala hilo, kwamba kwa nini hawakufanya mazoezi.


Badala yake, wachezaji walionekana ni wakali hata kupigwa picha tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic