June 12, 2018


Straika hatari wa Gor Mahia FC, Mganda, Meddy Kagere amehusishwa kuingia katika rada za mabingwa mara 27 wa Ligi Kuu Vodacom, Young Africans kwa ajili ya kumsajili.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa mabosi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na mshambuliaji huyo aliyekuwa gumzo kwenye michuano ya Kagame baada ya kuifunga Simba katika fainali ya SportPesa Super CUP.

Wakati taarifa zikieleza kuhitajika Yanga, mchezaji huyo amebakiza mwezi huu pekee na baada ya hapo anaweza akawasili Tanzania endapo mazungumzo ya pande mbili yataffikia mwafaka.

Ripoti kutoka Kenya zinaarifu kuwa Kagere amekubali kutua Tanzania endapo watakubaliana na Yanga kwa dau ambalo atalihitaji kutokana na mkataba wake kuelekea ukiongoni, na sasa yu huru kuanza mazungumzo ya kuelekea popote pale.

Mpaka sasa Yanga bado inasaka washambuliaji hatari kuziba ile safu ya ushambuliaji yenye mapengo kwa sasa iliyojulikana kama MTN (Msuva, Tambwe na Ngoma).

3 COMMENTS:

  1. Na huku hela hapana twanangoja kuchangishana

    ReplyDelete
  2. Hakuna Mganda anaitwa Meddy Kagere,uandishi wa ajabu ajabu

    ReplyDelete
  3. Usifanye haraka ya kutuwa, Yanga ndip kwanza inataksa inapitisha sanduku la kuomba ruzuku na ukija itabidi ungojee mpaka itakapopatikana ila ikiwa.umekaribishwa.na Simba au Azam, basi hata kesho unaweza kujs

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV