June 15, 2018





NA SALEH ALLY 
NILIANDIKA makala kuhusiana na Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr akieleza mambo mengi ambayo hakuwahi kuyasema wakati alipokuwa akifanya kazi Simba.


Kerr raia wa Uingereza alifanya kazi Simba na hakuwa na mafanikio kama ambavyo ilikuwa inatakiwa au mwenye alivyoaminimambo yangeweza kuwa hadi alipofukubwa.


Mara nyingi Kerr hakuwa anafurahishwa na uamuzi wa Simba kumuondoa huku akiamini mambo mengi yaliyozungumziwa kuhusiana nay eye na kutofanya vizuri hayakuwa sahihi.


Lakini mar azote, Kerr akaendelea kuwasifia mashabiki wa Simba akisema ni wenye subira kuliko timu nyingi na hatawasahau katika maisha yake ya kazi akiwa na klabu hiyo moja ya zile kongwe nchini.


Mara zote, Kerr alikuwa akilaumu sana kuhusiana na viongozi wa klabu ya Simba na mambo kadhaa. Hata hivyo hakuwa akiweka kila kitu hadharani kuonyesha namna mambo yalivyokuwa.

Baada ya michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika mjini Nakuru, Kenya, timu yake ya Gor Mahia ilifanikiwa kuchukua ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na sasa itasafiri kwenda England kuivaa Everton katika mechi ya kirafiki itakayopigwa kwenye Uwanja wa Goodison Park, Liverpool.


Kumaliza kwa michuan hiyo, kulimfanya Kerr kuwa gumzo kutokana na mafanikio mfululizo ambayo alishindwa kuyapata Simba na hata ikaelezwa wako waliamini angefaa kuisaidia Simba kama angerejea.


Mwenyewe akaonyesha hakuwa na kinyongo na Simba na kama akipata nafasi hiyo kwa makubaliano mazuri siku moja angerejea lakini msisitizo wake ukawa ni baadhi ya viongozi wa Simba asingekubali kufanya nao kazi.


Wengi aliokuwa akiona asingefanya nao kazi ni wale waliokuwa katika kamati ya utendaji. Baada ya hapo, Championi lilimchimba na kutaka kujua sababu hasa zilizomfanya kuona wasingefaa ni zipi.


Kwa maoni yake, Kerr aliamini viongozi hao hawakuwa waungwana, walikuwa watu wenye chuki na hawakufanya kazi kwa kuisaidia Simba badala yake wao wenyewe.


Kuthibitisha hilo, alizitaja sababu nyingi ikiwemo kufanya kazi nje ya weledi kama vile. Kuingilia kazi za kocha, mfano kupanga kikosi, kulazimisha wachezaji fulani wacheze, kutaka vitu ambavyo haviwezekani na kadhalika.


Mfano katika usajili, Kerr aliona kocha hakuwa akipewa nafasi ya kuchagua wachezaji aliowataka au kuwaona. Aliona kuna viongozi walikuwa wakilazimisha kusajiliwa kwa wachezaji waliowataka wao kwa mapenzi yao binafsi  au wanakuwa na biashara zao binafsi.


Alieleza namna ambavyo wachezaji ambao aliona hawafai wakisajiliwa na baadaye viongozi kulazimisha wachezaji hao wacheze wakati yeye kama kocha aliona hawakuwa na nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Nimefuatilia baada ya makala hiyo kwamba imewakwaza wengi sana hasa wale wenye hisia kwamba wanahusika au inawagusa. Wako walionipigia simu kuona kama wanaharibiwa wakiamini kocha hakuwa sawasawa.

Lakini wako wamezungumza na watu wengine wakinilalamikia kuona kama eti, Simba imetulia na mimi sasa naanzisha maneno yasiyofaa. Hizi ni hoja dhaifu na za hovyo kabisa na kwangu naona hawa ni wale walioguswa.

Simba haiwezi kuvurugwa na watu kuambiwa ukweli, Simba haiwezi kuvurugika kwa watu kuamua kujirekebisha na kuwa bora. Mfano unaambiwa ufanye kazi kwa maslahi ya Simba na si wewe binafsi. Hapa unavurugwa wapi?

Kulalamika ni kuonyesha kweli kuna tatizo. Kulalamika hakutakuwa tisho hata kidogo kuzuia kazi isifanyike ili kuwafanya watu fulani wasiguswe au kuambiwa ukweli.

Anayekuambia ukweli ni mwema kuliko anayenyamaza au akizungumza atakusifia tu. Huenda Kerr ni mtu mwema kwa Simba kwa kuwa anawaambia mambo mema kutokana na alichopitia.

Kama mtachukulia chanya na kulifanyia kazi, basi mjue hili linaweza kutengeneza njia bora zaidi katika mwendo wa Simba kwenye safari ya kurudisha heshima yake. Lakini mkiwa hasi na kuona mnaonewa, tatizo halitaisha milele na matatizo yataiganda Simba daima.

6 COMMENTS:

  1. Tatizo lako unaandika majungu au hearsay .Umehoji hao wanaotuhumiwa?Au kwa vile kasema Kerr basi ndio ukweli?Hivi kocha huyo ameondoka Simba siku za hivi karibuni?Mwandishi gani usijejua ethics za journalism kwamba lazima usikilize pande zote mbili ili upate ukweli. Watu wanatuhumu kwa sababu hufanyi kazi yako ipasavyo.Kusikiliza upande mmoja na kuhukumu ni umbeya, uchonganishi na majungu.Wahoji wanaotuhumiwa upate ukweli.


    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanafalsafa tuna kauli isemayo ukishindwa kubadilisha mfumo uliopo basi aidha badilika wewe kuendana na mfumo au achana na mfumo huo. Kerr alichagua kuachana na mfumo. Nakuunga mkono ndg, mwandishi analeta majungu imekuwa mazoea kwa waandishi kutuletea taarifa kuhusu viongozi hasa makocha wakitimuliwa. Chakushangaza viongozi hao hawatajwi kwa majina na kufanya yote kutokuwa na maana. Kutowataja maanayake unahofu na ulichoandika. Kusanya taarifa kuhusu kisa kutoka pande mbili utuletee conclusion. Vinginevyo mwandishi wa habari unakuwa mbabaishaji to.

      Delete
  2. Unajinasibu vipi kuwa unamwambia mtu ukweli wakati hujamtaja? Siwezi kuamini viongozi wote simba ni tatizo. Hao wanaotuletea matatizo watajwe basi. Kushikilia msimamo wa Kutowataja hauisaidii simba na ndo maana unaambiwa unataka kutuvuruga kwani unataka kutuaminisha kuwa viongozi wote ni tatizo.

    ReplyDelete
  3. kuna kizazi fulani hapa Tanzania kilinyimwa elimu kwa makusudi haya ndio matokeo yake wanashindwa kujadili hoja wanakimbilia matusi hawa utawakuta kila sehemu nenda kwenye siasa utawakuta hii ndio Tanzania

    ReplyDelete
  4. Mwandishi hujui maadili ya uandishi. Wala hujui uongozi bora. Unaandika kinachokupendeza wewe na ni mtu wa kujisifia na kujiona bora.

    ReplyDelete
  5. Napata tabu sana kuamini kwamba huyu mwandishi amesomea journalism. Unapopata habari au kufanya interview inayohusu pande mbili inabidi upate maoni ya pande zote mbili.Ethics za journalism haziruhusu kuandika habari ya upande mmoja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic