June 18, 2018




Baba wa kipa wa Singida United, Manyika Peter ambaye ni Peter Manyika, leo amepanga kuiandikia timu ya mwanaye barua ya kusitisha mkataba wa kuendelea kuichezea.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu usajili wa Ligi Kuu Bara ufunguliwe kwa klabu 20 shiriki za ligi katika msimu ujao huku mwanaye akiwa amebakiza mwaka mmoja.

Kipa huyo alijiunga na Singida msimu uliomalizika akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Manyika amesema kuwa amefikia hatua hiyo ya kuuvunja mkataba wa mwanaye Singida kutokana na kukiuka makubaliano yaliyokuwemo kwenye mkataba.

Peter alisema moja ya makubaliano hayo ni kutommalizia fedha ya usajili ambayo alitakiwa apewe kabla ya msimu uliomalizika kumalizika, hivyo kisheria Singida imevunja yenyewe mkataba.

“Kuna makubaliano mengi yameshindwa kutimizwa kwenye mkataba wa mwanangu Manyika pamoja na klabu yake anayoichezea ya Singida.

“Hivyo, kama baba ambaye mimi ni meneja wake ninayemsimamia katika soka, nimeona nichukue maamuzi ya kuiandikia timu yake ya Singida barua ya kusitisha mkataba wake.

“Na hilo la kuvunja mkataba lipo wazi kwani Singida wenyewe wamekiuka makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba kwa kushindwa kutimiza vitu vingi vilivyokuwepo kwenye mkataba ikiwemo fedha ya usajili ambayo bado hajamaliziwa,” alisema Peter.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic