June 13, 2018


Mchezaji wa kimataifa wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, amefunguka na kueleza kuwa mkataba wake na klabu yake unamalizika Julai 7 2018.

Wakati mkataba wake ukielekea kumalizika, Mavugo amesema Yanga ni moja ya timu zinazomuwinda hivi sasa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chake.

Mbali na kuhusishwa na Ssimba, Mavugo pia amesema ataendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na namna ilivyomlea tangu ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi endapo watamuongezea mkataba mwingine.

Aidha, timu za Singida United na Gor Mahia FC ya Kenya nazo zipo kwenye rada ya kutaka kumsajili mchezji huyo kwa ajili ya huduma ya msimu ujao.

Mavugo ameeleza kwa sasa yupo nchini kwao kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha timu yake ya taifa katika mashindano ya kufuzu kuelekea AFCON.

3 COMMENTS:

  1. Mavugo ni Ibrahim Ajibu wa burundi kwa kumuangalia hafla amekamilika hasa kwenye pysical structure yaani maumbile yao ya kimwili yanaonekana yapo kikazi zaidi lakini yanakosa akili yenye ubunifu ya jinsi gani ya kutumia uwezo wao wa mwili kuyatawala mazingira yao ya kazi. Kwa mwenye akili timamu na mwenye kujitambua huwezi kuachia sehemu yenye mazingira mazuri ya kazi kwa kutegemea sehemu isio na uhakika na uwezekano wa kulipwa hata mshahara wako wa mwezi. Kwa upande mwengine simba wanaweza kumtrade Mavugo na baadhi ya mchezaji mwenye uwezo zaidi nchini hasa beki kwa kutoa nyongeza ya ada kuliko kusubiri kuondoka bure kwani alishawagharimu vya kutosha wanahitaji kunufaika japo kidogo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nani anakubali kumnunua wakati mkataba wake unaisha? Tatizo lako umewazia tu kwa Yanga amekuambia timu kadhaa zinamuhitaji mojawapo Yanga.
      Mbona samba mkisikia tu mchezaji Yanga inamtaka mnakuwa mnaogopa sana raha ya mpira timu zote zikamilike ili ushindani uwepo na ndio hapo tutapanda kisoka lkn mna mawazo ya uoga ili labda mshinde kila ,waka.
      Angalia Azam wanavyosajili ndio ujue ushindani utakuwaje mwakani usiiwaze Yanga tu.

      Delete
  2. Mavugo kaisha aende kokote tuu..kwa simba tunayoitaka atakaa bench mwaka mzima na atatuingiza hasara..aende tuu hata Yanga..hatakuwa na effect.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic