Uongozi wa klabu ya Yanga umeibuka kivingine kuhusiana na mchezaji wa Gor Mahia FC, Meddy Kagere ukieleza kuwa si kweli wana mpango wa kumsajili.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkuu wa Kamati ya Usajili ndani ya klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema taarifa zinazoripotiwa kuwa Yanga wameanza naye mazungumzo si za kweli.
Nyika amefunguka kwa kusema yawezekana taarifa hizo zinaandikwa baada ya kuonekana akizungumza naye kwenye mashindano ya SportPesa yaliyomalizika siku chache zilizopita nchini Kenya.
Kiongozi huyo ameeleza kitendo cha kuonekana na Kagere wakiongea imechukuliwa kama ni mpango wa Yanga kukamilisha dili la usajili ili aweze kujiunga na timu hiyo.
Licha ya kusema hayo, siku kadhaa zilizopita Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa alisema ni kweli wana mazungumzo na Kagere ila muda mwafaka ukifika watauarifu umma wapi walipofikia.
Kauli ya Nyika inakuwa kama inaleta mkanganyiko juu yake ya Mkwasa kutokana na kila mmoja kuwa tofauti.
Sio mkanganyiko ila sema nyie waandishi ndo mnaandika habari zisizokuwa na utafiti ilimradi ni simba na yanga ili muuze. Hata mkwasa hakuwahi kukiri bali alisema sio wakati mwafaka kuzungumzia usajili, wakati ukifika mtaambiwa. Nyie andikeni habari za muro na akilimali tu maana ndo uwezo ulipoishia. Mkianza kutafiti, wala hamtaandika tena gossips
ReplyDelete