June 12, 2018








Katika msimu wa Soka ambapo kila mpenzi wa Soka duniani anayo matarajio makubwa na timu anayoishabikia, StarTimes inakuletea Ofa Kabambe ya Damka na StarTimes App ambapo mteja atapata Michuano ya Kombe la Dunia kwa 3500 tu atakapotumia StarTimes App inayopatikana PlayStore kwa watumiaji wa Android na AppStore kwa watumiaji wa IOs (Iphone).

Kampuni ya StarTimes ndiyo kampuni ya kwanza Tanzania kuleta mapinduzi ya kidigitali na hii sasa inakuwa ni hatua nyingine kuelekea Mapinduzi mapya kwa teknolojia ya vipindi kwa njia ya simu. 


Na kwa msimu huu wa Kombe la Dunia waateja na wasio wateja wa StarTimes kwa pamoja wanaweza kuangalia michuano hiyo kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh. 3500 tu kupitia StarTimes App.

Akiongea katika Uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa alisema, “Ni wazi wengi wetu tumeshuhudia jinsi ambavyo gharama za Internet ziko ghali hasa unapotaka kufanya “Live Streaming”. 

Kwa kupitia teknolojia ya App yetu, wateja wetu watatumia kiasi kidogo sana cha data. Huu ndio wakati wa kwenda kidigitali zaidi Pakua App yetu sasa, kuwa miongoni mwa wateja 20,000 wa kwanza kujiunga na StarTimes App na utalipia 3500 tu”.

“Kwa 3500 hiyo utapata mechi zote 64 MUBASHARA kiganjani mwako tena kwa Siku 38, kwa kiwango cha screen utakachopenda wewe iwe SD, HD au Ultra-High Definition (UHD) chaguo ni lako. Baki na Sisi Soka limenoga”. Aliongeza Malisa.


Ofa hii ni kwa wateja 20,000 tu watakaopakua StarTimes App kabla ya tarehe 14 Juni yaani Alhamisi ya wiki hii. Kombe la Dunia linaanza siku hiyo hiyo ya Alhamisi ambapo StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo inayofanyika nchini Russia.


1 COMMENTS:

  1. AZAM TV TU.....NA SISI TUNAPENDA UZALENDO NYIE KAMA WACHINA ENDELEENI NA UWAKALA WENU. AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP, AZAM TV APP

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic