June 18, 2018




Vile vipigo ambavyo imekuwa ikivipata timu ya wanawake ya Simba, Simba Queens, vimewashtua viongozi wa Simba na kusema kuwa ni somo kwao, hivyo wanajipanga kufanya maboresho zaidi msimu ujao.

Simba Queens imecheza mechi tisa katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara lakini imeambulia ushindi mmoja tu huku ikipokea vipigo nane na kutia aibu katika ligi hiyo.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, Said Tully, alisema kuwa wamefanikiwa kutimiza malengo ya kuifikisha timu kwenye ligi kuu ila bado kuna upungufu kidogo unaotokea ambao ni sehemu ya kujifunza.

“Timu yetu ya Simba Queens ni msimu wake wa kwanza kupanda ligi, hivyo kuna changamoto ambazo zipo kwetu, ni somo, tunajifunza na matokeo mabaya ambayo tunayapata kwa kweli yanatuumiza, mipango yetu ni kufanya timu iwe ya ushindani.

“Kutokana na matokeo yake kutoridhisha, uongozi unafanyia kazi upungufu uliopo ili kuweza kufikia zaidi malengo yetu ya kuwa na timu yenye ushindani,” alisema Tully.

Mshambuliaji wa Simba Queens, aliyepata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike katika Tuzo za Mo Simba Awards, Zainabu Rashid Pazzi, ambaye ana bao moja tu kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, alisema katika hafla hizo kuwa, timu yao inafanya vibaya kutokana na ukata.

“Nakuomba mheshimiwa Mo utuangalie na huku upande wa pili, hali ni ngumu, ndiyo maana timu haifanyi vizuri,” alisema Zainabu katika hafla hizo.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic