June 18, 2018




Na Fahad Ally

Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude atapumzishwa katika michuano ya Kombe la Kagame, mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza, Mkude atapumzishwa kutokana na kutumika sana.

"Katumika sana, anastahili kupumzika kwa kuwa baada ya hapo Simba itakuwa na michuano mingi sana.

"Kumbuka kuna suaka la kambi pia, hivyo ni lazima apate muda wa kupumzika pia," alisema mtoa taarifa.

Amesema pamoja na Mkude wachezaji wengine kadhaa pia watapumzishwa.

"Sijajua ni kina nani, lakini wako wengine ambao watapumzishwa. Ni suala ambalo nakuhakikishia litakuwepo."

Wakati wa michuano ya SportPesa Super Cup, Simba iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wake akiwemo John Bocco aliyekuwa majeruhi, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi na Waghana wengine wawili, Nicholas Gyan na James Kotei.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic