June 15, 2018




Kikosi cha mabingwa wa Tanzania, Simba taratibu kimeanza kusaka beki wa kati.

Taarifa zinaeleza, Simba imeanza zoezi hilo ndani na nje ya Tanzania kuhakikisha inapata beki wa uhakika wa kati.

“Kazi imeanza, wanapitia CV mbalimbali lakini leo ni kupata beki wa uhakika ambaye ataaminika.


“Unajua Simba ina mabeki wazuri lakini ugumu wa mashindano tunayokwenda nao una shida yake. Hivyo kazi inaendelea kwa utaratibu sahihi,” kilieleza chanzo.


Inaonekana kama mabeki wa Simba hasa Yusuf Mlipili wamekuwa wakipata kazi ngumu katika michuano ya kimataifa kutokana na uzoefu.

Ndani ya Simba kumekuwa na majadala kuhusiana na kubaki au kuachwa kwa beki Juuko Murshid ambaye inaonekana Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre hakumkubali kabisa.

8 COMMENTS:

  1. Unajua pale Simba wakati mwengine ni watu wa kushangaza sana. Makosa yanayotakwa kufanywa kwa Juko ndio makosa yaliyofanyika kwa Yondani na Amis Tambwe. Kuelekea mashindano ya kimataifa Simba wanachotakiwa kufanya ni kutafuta beki wa nguvu wa kuja kusaidiana na Juko lakini sio kutafuta mbadala wa Juko. Wakija kuteleza kuachana na Juko itakuwa moja ya makosa makubwa hasa ikishindakana kumpata beki zaidi yake.kwa kawaida masenta beki wengi duniani mara nyingi ni wachezaji wenye mazingira ya utatanishi sio rahisi sana kumpata senta beki amabae asilimia mia100 yuko sawa kitabia na kikazi kwa wakati mmoja. Simba wanatakiwa kuacha siasa kwamfano walimleta Gayani kama forward lakini inaonekana kashindwa kufiti sasa kwanini wasimtafute anaefiti akaziba nafasi yake?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama wewe kweli ni mfuatiliaji mzuri wa soka utagundua kuwa misimu miwili iliyoisha Juuko hajawa kwenye kiwango chake kile cha msimu aliokuja simba. Amekuwa akicheza kwa makosa ya ovyoovyo sana kama beki wa kimataifa hapaswi kufanya vile. Baada ya msimu wa kwanza Simba, ameota mapembe na kiburi hadi mazoezini kuwa anakosa. Mara anchelewa kambi n.k, Uwanjani ancheza madhambi ya kipuuzi sana. Joseph Omog na Lechantre wote hawajafurahishwa naye, wote wanapendekeza kuachwa. Hilo linatosha kukuonesha kuwa hafai kuichezea Simba

      Delete
  2. viongozi wa Simba wajinga sana Mpili bado mchanga na ametugharimu mechi nyingi lakini bado wana,pa nafasi mbele ya JUUrko angalia mechi na Lipuli na mechi na Gor Mahia magoli yote yalitokea kwa uzembe wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlipili ni moja ya mabeki wazuri sana huu ulikuwa msimu wake wa kwanza kuchezea timu kubwa, kasaidia kwa kiwango cha hali ya juu sana. anastahili kuendelea kubaki msimbazi

      Delete
  3. Mimi nilitaraji kuona kikosi kinaimarishwa badala ya kubomolewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wachezaji wamekamilia idadi huwezi kuimarisha bila kuondoa baadhi

      Delete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Kama Juko waganda wanamuamini na timu yao ya taifa tena kwenye mechi nzito tu kama ile zidi ya Misri na kuonesha kiwango bora kabisa hasa ukichukulia alikuwa akiwadhibiti kati ya washambuliaji bora kabisa kwa sasa dunianai kama akina Mohamed salah alafu simba wanashindwa kumuamini Juko kumkaba adam salama wa lipuli? Sasa hapo wewe mwenyewe kama akili zako ziko sawa tafakari. Juko inawezekana ana matatizo yanayochangiwa na mambo mengi hasa maslahi ni kitu cha Simba kukaa nae na kujua kwanini hayoko sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic