June 13, 2018


Wakati Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akiwapa Yanga saa 48 kwa ajili ya kutengua maamuzi ya kujiondoa katika mashindano ya KAGAME, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, amesema bado hawajajibiwa barua yao.

Karia aliwataka Yanga kutengua maamuzi hayo ndani ya saa tajwa hapo juu ambazo tayari zimeshapita kupitia barua iliyotuma shirikishoni ikieleza kuwa hawatoshiriki michuano hiyo ili kuwapa mapumziko wachezaji wao.

Mkwasa ameeleza kuwa tangu watume barua yao TFF bado mpaka sasa hawajaweza kupewa majibu huku msimamo wake ukiwa palepale kuwa hawatoweza kushiriki KAGAME.

Katibu huyo amesema hawana namna sababu wachezaji wao wa kimataifa wameshasafiri kuelekea kwao huku wa kikosi cha pili wakishiriki mashindano ya Uhai CUP mjini Dodoma hivyo itakuwa ngumu kushiriki.

Katika mashindano hayo, Yanga imepangwa kundi C ambalo lina timu za Dakadaha ya Somalia, St. George ya Ethiopia pamoja na watani zao wa jadi Simba SC.

1 COMMENTS:

  1. Yanga kwa makusudi imewapa livu wachezaji wake na kuwaruhusu wa nje kusafiri makwao na huku wakijuwa kuwepo kwa mashindano muhimu ya Kagame pale walipojuwa tu kuwa wamepangwa kundi pamoja na Simba bila kwanza kuchukuwa muongozo kutoka TFF ili iwe hayumkiniki kikosi chao kujiunga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic