June 12, 2018

Shabiki maarufu zaidi wa Simba, Said Hamis maarufu kama Muchacho ameibuka na kusema klabu yake ya Simba, haikumtendea haki wakati wa tuzo zilizoanzishwa maarufu kama  Mo Awards.

Muchacho ameiambia SALEHJEMBE kwamba katika kipengele cha mhamasishaji bora alichoshinda Msemaji wa Simba, Haji Manara, kwake anaona haikuwa sahihi.

"Hawakunitendea haki, hata kama ni tuzo za msimu uliopita, Manara si mhamasishaji, ni msemaji. Si mtu anayekaa jukwaani kuhamasisha, anazungumzia masuala ya klabu na nini kinaendelea

"Mtu anayezungumzia usajili, safari ya klabu anahamasishaje? Mimi ndiye mhamasishaji, si uliopita tu, ni msimu yote na leo utaona wimbo wa Kidede ndiyo maarufu zaidi kuliko mingine yote ya Simba," alisema Muchacho ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kundi kongwe zaidi la ushangiliaji la Simba la Muchacho.

"Nimeona hadi wasanii wamewapa tuzo, hivi ni kweli kwa kuwa tu wameposti kwenye mitandao ya kijamii?"

"Achana na kutonituza, angalia hata mwaliko tu kweli. Kama nilikuwa kati ya wanaowania tuzo, walishindwa kunialika nifike pale? Hili ndiyo limeniumiza zaidi, nimehangaika sana na Simba."

Mzee Muchacho ametoa mipango mingi ikiwemo kuendelea kuhamasisha kuhusiana na Simba licha ya kuwa na umri mkubwa, jambo analoamini walipaswa kulifikiria pia.

"Kuhusiana na wachezaji, kweli niwapongeze Mo Awards, maana itawasaidia kujituma na kujua kila mwisho wa mwaka kuna tuzo.

"Maana kama unaona mwenzako amepewa tuzo safari hii, basi utajituma ili uipate safari nyingine, kwenye hilo wamefanya jambo zuri sana."

.


2 COMMENTS:

  1. Mimi nakubali maoni kwamba lile kundi la Kidedea ni wahamasishaji wazuri walistahili kutambuliwa, lakini huu ni mwanzo wapo wengi waliostahili Tuzo haiwezekani wote wapate, tuwe na subra.

    ReplyDelete
  2. Patience is bitter, but its fruits are sweeter

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV