July 7, 2018


Licha ya kuandika barua ya kujiondoa katika uteuzi wa Kamati Maalum ya kuisaidia Yanga wakati wa mpito, kiongozi wa zamani wa klabu hiyo, Abdallah Bin Kleb, amesema ataendelea kutoa msaada wake, imeelezwa.

Kleb ambaye aliwahi kuiongoza Yanga miaka kadhaa nyuma ameandika barua kwenda Yanga iliyoeleza kujiondoa kwake kwasababu ya kutingwa na majukumu ya kikazi pamoja na hali yake kiafya kuwa si rafiki.

Mbali na kutuma barua hiyo, imeelezwa kuwa Kleb amefunguka na kusema kuwa atakuwa anaisaidia Yanga kwa kile atakuwa anacho kwani amekuwa sehemu ya msaada ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu.

Kleb ameeleza kujiondoa kwake katika nafasi hiyo si kwamba ndiyo ameacha rasmi kujitoa kwa ajili ya klabu hiyo kongwe na badala yake atakuwa anajitahidi kuichangia kama mwanachama.

Kleb aliteuliwa na Yanga kuwa mmoja wa wajumbe maalum wa kuivusha na kuisaidia klabu wakati huu wa mpito inaoupitia kupitia Mkutano Mkuu wa klabu uliofanyika mwezi Juni 2018.

2 COMMENTS:

  1. Wanachokitaka yanga Binkleb ni musaada wa pesa tu si kitu chengine na ndio akajiamulia kujitenga kabla hajafilisika

    ReplyDelete
  2. Hewe Binkleb ameshndwa Manji utaweza wewe. Jishughulishe na biashara zako za kukuendeshea maisha wasije wakakumaliza baba wa watu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic