August 20, 2018


Yusuf Manji amerudi na Yanga imeshinda dhidi ya Waarabu. Ndiyo, kikosi cha Yanga jana kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, mabao ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 43 na Heritier Makambo (47), huku lile la USM Alger likifungwa na Abderrahmane Meziane dakika ya 57.

Kabla ya mchezo huo, aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji aliwasili uwanjani hapo kutoa hamasa kwa wachezaji wa timu hiyo. Manji ambaye aliingia Uwanja wa Taifa majira ya saa 11 jioni, alianza kwa kusalimiana na mashabiki wa Yanga kabla ya kuingia kwenye vyumba vya wachezaji na kuzungumza nao kwa dakika kadhaa.

Yanga iliyopangwa Kundi D, katika mechi tano ilizocheza mpaka sasa, imepoteza tatu, sare moja, huku ikishinda moja. Imebakiwa na mechi moja dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Sasa imefikisha pointi nne katika kundi hilo, hivyo haiwezi kusonga mbele, na bado ipo mkiani. 

Ikumbukwe kuwa, Juni 15, 2016, Manji alitangaza kujiweka pembeni kwenye nafasi yake ya uenyekiti ndani ya Yanga, lakini Julai 13, mwaka huu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia rais wake, Wallace Karia, lilitangaza kumtambua Manji kuwa ndiye mwenyekiti wa Yanga na haitambui kujiweka kwake kando.

Manji jana alionekana uwanjani akiwa pembeni ya Karia katika eneo la watu wazito, na baada ya mchezo huo, alirudi tena vyumbani kuzungumza na wachezaji akiambatana na mgeni rasmi wa mchezo huo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic