KIONGOZI SIMBA AIBUKA NA TAMKO BAADA YA MECHI VS MBAO ALHAMIS
Baada ya kupoteza mchezo wa ligi juzi Alhamis dhidi ya Mbao FC, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amewataka mashabiki wa timu hiyo kushusha presha chini.
Rage ameeleza kuwa ifikie hatua wanasimba waelewe kuwa katika mpira hakuna timu inayoshinda siku zote bali kuna siku lazima ipoteze ama iende suluhu.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mashabiki wa timu hiyo kuanza kuutupia lawama uongozi kutokana na kupoteza jambo ambalo liliepekea kutupiwa chupa kwa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara.
Rage amewaomba wanasimba kushusha presha chini na kuchukulia kuwa ni hali ya mchezo hivyo ni vema wakatuliza munkari kwa kuwa timu ina kikosi kizuri.
Kiongozi huyo amewashauri wanasimba wote kuwa wapole kwani anaamini kikosi kitakuja kufanya vema zaidi siku uzoni kutokana na namna ilivyosajili.
Kufungwa kwao ni matokeo ya wachezaji wengi kutojitambua vizuri. Simba wawe na mpango wa kuwapa counselling wachezaji wajue thamani ya club na wao wenyewe.
ReplyDelete