KOCHA ZAHERA AIBUA MSALA YANGA
Kocha Mkuu wa Yanga ameendelea kuwa mbogo kwa wachezaji wake baada ya kueleza kuwa mchezaji yoyote atayeleta utovu wa nidhamu ni lazima ampige chini.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kwuaondoka kambini hivi karibuni wachezaji wa Yanga ikiwemo Ramadhan Kabwili ambaye mpaka sasa hajarejeshwa kikosini.
Kocha huyo kutoka Congo, amesema kwa sasa anahitaji wachezaji wake kufuata masharti ili waweze kuendana na kasi yake kwani hataki mzaha kabisa kwa yoyote yule.
Zahera amesisitiza hilo ikiwa ni baada ya kuwasamehe Said Makapu, Pius Buswita na Mwinyi Haji ambao aliwafukuza hivi karibuni kambini kwa utovu wa nidhamu.
Kauli hiyo sasa inakuwa kama msala kwa wachezaji wote ambao wamekuwa wavivu kuwasili mazoezini mapema pamoja na suala la nidhamu ambalo hataki kuona yoyote yule akikiuka.
Wakati huo Zahera amezidi kuifua Yanga kuelekea mechi yake ya ligi dhidi ya Singida United Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nidhamu Ndio Siri ya Mafanikio
ReplyDelete