MAGUFULI AMCHARUKIA MBOWE “USITAFUTE KIKI AJALI MV NYERERE”- VIDEO
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaonya wanasiasa kutumia tukio la msiba wa jali ya MV Nyerere kutafutia kiki za kisiasa kana kwamba wanafahamu ajali hiyo ilivyotokea.
Magufuli amesema hayo leo jioni wakati akitoa salam za pole kwa Taiofa kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana na kuua jumla ya watu 131 wamepoteza maisha huku wengine 40
wakiokolewa.
Kauli hiyo ya rais imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuzungumza na vyombo vya habari na kumtaka Rais awawajibishe wote waliohusika na tukio hilo huku akiilalamikia serikali kwa madai ya kushindwa kufanya juhudi za uokoaji kwa jana na kusitisha zoezi hilo hadi leo kutokana na giza.
Mbali na Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia naye alitoa kauli akiitaka serikali kuboresha mindombinu ya uokoaji na kutoa elimu hiyo ikiwa ni sambamba na kuanzishwa kwa chombo maalum cha kupambana na maafa.
Aidha, Rais ameagiza Bendera ya Taifa kupepea nusu mlingoti kwa siku nne kuanzia leo Septemba 21 hadi Septemba 24, kufuatia ajali hiyo na kuagiza wahusika wote wakamatwe na kuhojiwa na watakaokutwa na hatia wachukuliwe hatua.
0 COMMENTS:
Post a Comment