VIDEO: MV NYERERE UPDATES: MIILI INAOKOLEWA, WALIOKUFA WAFIKIA 100 – VIDEO
Zoezi la uokoaji wa miili ya watu waliozama katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere linaendelea muda huu ambapo vikosi maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi, JWTZ , Jeshi la zimamoto na uokoaji na wazamiaji kutoka kampuni ya huduma za ndege Mwanza kusitisha zoezi jana usiku kutokana na ukosefu wa vifaa vyenye uwezo wa kufanyakazi kwenye giza.
Kwa mujibu wa HABARI ZA MIKOANI kutoa TBC 1, imeelezwa kuwa mpaka leo asubuhi, waliookolewa wakiwa wamepoteza maisha idadi yao imeongezeka na kufikia 79.
Mpaka jana usiku, watu 44 walikuwa wameokolewa wakiwa wamepoteza maisha huku 37 wakiwa majeruhi lakini hali zo zilikuwa mbaya.
RC wa Mwanza, John Mongela amesema idadi ya watu waliofariki kwa ajli ya #MvNyerere kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 94 leo asubuhi na mpaka kufikia majira ya mchana huu saa nane imefika 100. DC Ukerewe amesema Kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kibeba abiria zaidi ya 400.
Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio kuongeza kasi ya kuokoa na kuopoa watu waliopinduka na kivuko hicho. Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Simon Sirro na Waziri wa Uchukuzi Isaac Kamwelwe wamefika eneo la tukio kushiriki uokoaji.
Wakati uokoaji na uopoaji ukiendele mamia ya wakazi wa visiwa hivyo wamefurika kituo cha afya cha Bwisya kutambua jamaa zao walioopolewa.
Tayari uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.
Uzembe huu yani mpaka aibu.Baada ya ajali ya mv Bukoba Dunia na watanzania wengi waliamini wahusika wangejufunza kutokana na makosa ili ajali za kizembe kama hizi zinazopoteza mamia ya maisha ya watu hazitokei tena. Chanzo cha ajali ni chombo kubeba abiria na mzigo kupita uwezo wake ni makosa yale yale.Imekuwa ni kitu cha kawaida kabisa kuona mabasi na vyombo vyengine vya usafiri vikijaza kupita uwezo unaoruhusu. Imekuwa kawaida kuona bodaboda ikitunga mshikaki. Hii ajali ni doa kubwa katika serikali ya awamu ya tano licha ya jitihada kubwa ya muheshimiwa raisi kuhakikisha kila mtu anawajibika kikamifu katika sehemu yake ya kazi lakini bado inaonesha yakwamba uzembe na wazembe ndani ya serikali na watendaji wake ungalipo tena kwa kiwango cha kutisha. Wenzetu Wachina na serikali yao katika matokeo ya ajali kama hizi za kizembe zinazosababishwa na watendaji wazembe huwa hawana kupepesa macho katika kutoa adhabu za fundisho. Huwa wananyonga tena hadharani. Haya mambo ya kwetu kuleana leana kipumbavu bila ya adhabu stahiki ndio vyamzo ya maafa yote haya. Kwani hili ziwa lipo Tanzania peke yake? Na kwanini ajali zitokee upande wetu tu? Kwakweli ni ujinga kabisa na hicho kivuko kina jina la baba wa taifa hakuna jengine isipokuwa ni kulinajisi jina la muasisi wa Taifa katika misingi ya kibiashara kwa chombo kilichokuwa kinaendeshwa na watu wa hovyo bila ya kujali maisha ya watu. Kwa wenzetu taasisi au mahala panapopewa majina ya waasisi wao wa taifa huwa sio vitu vya mchezo mchezo lakini kwa kwetu ndio kama tunavyoshudia yanayottokea. Hi nchi ina watu vichwa ngumu sana tena wa hovyo na bila ya maamuzi ya kidikteta kupambana na uzembe wa namna hii sidhani kama wahusika wataelewa. Si shauri kiongozi wetu mkuu wa nchi awe Dikteta lakini raisi wa Philippines tayari ameshanyonga karibu watu alfu nne kama adhabu kwa watu walio jihusisha na makosa mbali mbali hasa ya madawa ya kulevya. Licha ya jumuia za kimataifa kulani kampeni yake hiyo lakini raisi huyo amesema hatakoma kuendelea na vita yake hiyo ya kuieka sawa nchi hiyo kwani ilishafika pabaya na hakuna mwenye uchungu wa raia wake kupoteza maisha kama yeye ila idadi ya hiyo ya watu zaidi ya elfu waliouwawa ndani ya mikono ya serikali yake walikuwa wanaenda kungamiza karibu maisha ya wafipino wote kwa hiyo kuwahi kuwaondosha wao kabla ya kuleta madhara kwa watu wengine kwake yeye aliona ni sahihi kabisa.wakati mwengine lazima kuwe na maamuzi magumu bila ya kuchelea ili kunusuru maisha ya watu la sivyo tutalia kila siku.
ReplyDeleteKiswahili ni lugha yetu adhimu na waandika habari wanapaswa kuienzi. Ikiwa Miili ya ndugu zetu inaokolewa je manusura wanafanywaje?
ReplyDeleteSishangai mara nyingi mahala pa R niikutapo L!!!