September 21, 2018


Kiungo Mrwanda anayekipiga katika klabu ya Simba, Haruna Niyonzima, amesema ana mechi tano pekee za kuamua kuendelea ndani ya timu hiyo au la, kuliko kuendelea kutocheza, imeelezwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Niyonzima ambaye hajacheza mechi nyingi ndani ya mabingwa hao watetezi, amesema atavunja rasmi mkataba wake endapo ataendelea kuwekwa benchi.

Kiungo huyo aliyewahi kuichezea Yanga ameamua kuvunja ukimya na kueleza kuwa atafikia maamuzi hayo kutokana na kujiamini juu ya kiwango chake kuwa bado ana uwezo mkubwa wa kulisakata kambumbu.

Niyonzima ameeleza ni vema zaidi akifanya hivyo kuliko kuua kiwango chake ili kulinda heshima aliyonayo ndani ya soka la Tanzania.

Hivi karibuni mabosi wa Simba walikutana na mchezaji huyo kumaliza tofauti baina yao baada ya kuchelewa kuripoti kambini na pia kukosa ziara ya Uturuki ambayo timu ilikaa kwa wiki mbili.

3 COMMENTS:

  1. Sasa nani wakulaumiwa kama si yeye mwenyewe binafsi? Kwanini alishindwa kuungana na timu kwenye maandalizi ya awali ya Timu? Anataka kocha amapange kwa sababu ya Jina lake na sio kiwango chake kwa Simba hii atasubiri sana. Tuwe wa kweli Simba imefanya kila inaloweza kumsapoti Niyozima kama vile kumuhangaikia katika kuhakikisha afya yake inarudi katika hali ya kawaida baada yakupata majeraha. Sasa kama anataka kuuvunja mkataba na Simba hilo ni suala linalotaka kufuata sheria na sio kukurupuka.

    ReplyDelete
  2. AONDOKE ZAKE UPUUZI HUO YEYE NDIYE TATIZO

    ReplyDelete
  3. AVUNJE AWALIPE SIMBA HELA YE ANAJIONA SUPASTAA KWAMBA ASIHUDHURIE MAZOEZI HALAFU AKIJA APANGWE HII SIO YANGA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic