RAIS CAF ATUMA SALAAM ZA POLE KWA MSIBA MZITO MV NYERERE MWANZA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad kupitia Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi msiba wa waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama jana kati ya Ukara na Bugorara,Ukerewe.
Rais wa CAF Ndugu Ahmad ametoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Muheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli na Watanzania kiujumla.
Ametoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa msiba huo mzito uliosababisha majonzi makubwa kwa Watanzania.
“Naungana na Watanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Muheshimiwa John Magufuli kwa msiba huo mzito kwa Tanzania” alisema Rais wa CAF Ndugu Ahmad
Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Wallace Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki wa waliofariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama kati ya Bugorara na Ukara wilayani Ukerewe.
Rais wa TFF Ndugu Karia amesena ni huzuni kubwa kwa Taifa na Watanzania kwa ajali hiyo iliyopoteza wapendwa wetu.
Amesema ajali hiyo imepoteza wana familia ya Mpira wa miguu ambao walikuwa wakifuafilia ama mashabiki wa mchezo huo lakini pia ajali hiyo imepoteza nguvu kazi ya Taifa.
TFF inaungana na Ndugu,jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupoteza wapendwa wao.
Pia TFT inawapa pole na kuwatakia afya njema majeruhi waliookolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana.
Mungu awalaze mahali pema peponi wale wote waliopoteza maisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment