September 21, 2018


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limeahirisha mechi za Simba dhidi ya Biashara United pamoja na Yanga dhidi ya JKT Tanzania Tanzania.

Yanga ilitakiwa kukipiga na JKT Septemba 26 2018 wakati Simba ikipaswa kucheza na Biashara Septemba 27 mechi zote zikafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa zitapangiwa tarehe nyingine.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya uongozi wa Simba kutuma maombi ya kuomba mechi yao na Biashara United isogezwe mbele ili kuwapa nafasi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah, alieleza wameamua kuomba mechi na Biashara iahirishwe ili wapate muda mzuri kujiwinda na Yanga kwa maana ratiba itakuwa inawabana.

Baada ya maombi hayo kufika TFF, imeelezwa taayari wameridhia maombi hayo na sasa mechi hiyo itapangiwa tarehe nyingine pamoja na ile ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania.

5 COMMENTS:

  1. Ndio ujinga mtupu. umewahi kuona wapi tangu Dunia iumbwe timu inapangiwa mechi 12 mfulizo katika uwanja wake wa nyumbami?

    ReplyDelete
  2. Huu no upumbavu was kiwanfo cha Phd, kwani mechi ya Yanga na Simba sio za ligi kuu!? Hivi mtibwa, Azam, Mbao na wengine wakiomba itakuwaje!? Kwani JKT na Biashara wapewe adhabu bila sababu!!? Mbona sijawahi kusikia Barca vs Real au Arsenal vs Man nk zikiahirishwa!!?

    ReplyDelete
  3. na kumbuka timu ya Njombe mji iliomba kubadilishiwa ratiba lakini wakagomewa leo Simba wanaomba wanakibaliwa tena ya Njombe mji ndo ilikua ngumu zaidi kwani ilikua ni mikoa tofauti. OK all the best TFF

    ReplyDelete
  4. Hapo kichwa cha habari kinasema Simba imebadilisha ratiba ya TFF.Na kwa nini siyo Yanga imebadili ratiba kama nao mechi yao na JKT imebadilishwa.Unajua mwandishi wewe unacheza na akili za watu.Acha kuwa unaandika habari ambazo zinaonyesha wewe ni timu gani...upuuzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic