October 18, 2018


Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma ambaye aliwasili nchini October 2017 akichukua nafasi ya Jose Mayanja, amepata shavu la kuinoa timu ya As Kigali  inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda. 
 Djuma alikuwa kocha msaidizi Msimbazi, anakuwa kocha mkuu ndani ya timu  mpya ambayo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja mara baada  kocha mkuu wa timu hiyo Eric Nshimiyimana kujiuzulu.
Timu nyingine ambayo ilikuwa ikihitaji saini ya Djuma baada ya  kuachana na Simba kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems ni Inter Class ya Burundi ambayo inashiriki ligi daraja la pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic