October 17, 2018


Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe amemkingia kifua nahodha wa timu ya Taifa Mbwana Samatta kwa kukosa penati kwakuwa ni sehemu ya mchezo ila hajaridhika na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).


Mwakyembe alisema kuwa kwa ushindi huo wamerejesha imani kwa watanzania pamoja na furaha licha ya kukosa nafasi ambazo walizitengeneza ndani ya uwanja .


"Achana na suala la kukosa penati,hiyo ni sehemu ya mchezo ila wameonyesha namna ambavyo thamani ya bendera ya taifa inakuwa hasa kwa kupata ushindi  katika uwanja wa nyumbani.

"Tulipaswa tufunge mabao mengi mpaka matano ila yote ni matokeo , bado tuna nafasi ya kuweza kusonga mbele wachezaji wanatakiwa waendelee kuonyesha juhudi  watanzania wanawafuatilia ,lengo ni kuweza kufuzu."alisema.



2 COMMENTS:

  1. huyu waziri wa michezo huwa anaongea pale stars inapopata ushindi ila ikifungwa anakaa kimya hawa ndio aina ya viongozi tulionao wanapenda sifa zaidi

    ReplyDelete
  2. Na kama waziri wa michezo inakuwaje kiongozi na mdau mkubwa kama Mohamed Mo anapotea halafu anakaa kimya? Hatujamsikia kusema lolote lile?mwakyembe anabifu Simba au nini kinaendelea?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic