October 17, 2018



LIPULI FC ya Mkoani Iringa hali siyo nzuri ya kifedha ni baada ya kushindwa kuwalipa wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo mishahara ya miezi miwili huku wakitishia mgomo.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kutafuta udhamini baada ya Vodacom waliokuwa wanadhamini Ligi Kuu Bara kujitoa. 


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, hali ni mbaya katika timu hiyo hali itakayosababisha wachezaji kugomea mazoezi kutokana madai ya mishahara hiyo.
Mtoa taarifa huyo alisema, tofauti na mishahara wapo baadhi ya wachezaji bado wanadai fedha zao za usajili ambazo bado hawajamaliziwa hadi hivi sasa. 


“Kiukweli hali ni mbaya Lipuli na hakuna haja yoyote ya kuficha, kama Yanga ambayo ni klabu kubwa nchini inalia ukata ikichangishana fedha itakuwa Lipuli. 



“Hivyo, tumeona tuliweke wazi hili ili yasije kujitokeza mengine makubwa ikiwemo wachezaji kugoma kufanya mazoezi na hata kucheza mechi za ligi, tunawaomba wadau wa soka wa Iringa kuisapoti timu yao,’alisema mtoa taarifa huyo. 


Alipotafutwa Katibu Mkuu wa timu hiyo, July Leo kuzungumzia hilo alisema kuwa “Ni kweli hali mbaya ya kiuchumi ipo Lipuli nikiri katika hilo, lakini ninaamini siyo kwetu pekee, kila timu ina hali mbaya kama yetu sisi. 


“Ninaamini ni hali ya mpito iliyokuwepo katika timu yetu, kama unavyofahamu ligi inachezwa bila mdhamini, nafikiri ni wakati wa TFF ambao ndiyo wadhamini na baba katika soka kutafuta udhamini kwani mambo ni magumu,”alisema Leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic