October 16, 2018





Mchezo umemalizika, Taifa Stars inapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde.
Dk ya 95: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka Samatta anaingia Rashidi Mandawa.

Dk ya 92: Cape Verde wanaongeza kasi ya kushambulia, wanafika langoni mwa Stars.
Zinaongezwa dakika 5 za nyongeza.
Dk ya 90: Stars wamepunguza kasi ya kushambulia, mashabiki wanaongeza kasi ya kushangilia wakiamini ushindi uko upande wao.

Dk ya 87: Msuva yupo chini kaumia, anapatiwa matibabu. Mchezo umesimama kwa muda.
Dk ya 84: Cape Verde wanapata kona, inapigwa Manula anadaka.
Dk ya 82: Samatta yupo chini, ameumia, watoa huduma wanaingia wanamtoa nje.
Dk ya 77: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Dk ya 82: Samatta yupo chini, ameumia, watoa huduma wanaingia wanamtoa nje.

Dk ya 74: Manula yupo chini baada ya kuumia wakati akiokoa mpira, mchezo umesimama kwa muda.
Dk ya 70: Mchezo ni mkali na timu zote zinashambuliana kwa zamu.


Dk ya 67: Taifa Stars wanafanya shambulizi kali lakini beki wa Cape Verde anafanya kazi nzuri kwa kuokoa krosi ya Samatta.
Dk ya 66: Cape Verde wanapata kona.
Dk ya 65: Himid Mao wa Stars anachezewa faulo, inapigwa kuelekea lango la Cape Verde.
Dk ya 64: Stars wanapata nafasi shuti linapaa juu ya lango.
Dk ya 60: Cape Verde wanapata faulo karibu na lango la Taifa Stars.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 53: Cape Verde wanapata mpira wa kurusha.
Dk ya 52: Abdi Banda ametoka, nafasi yake imechukuliwa na John Bocco.
Dk ya 50: Cape Verde wanapata kona, inapigwa inaokolewa na walinzi wa Stars

Dk ya 48: Mchezo umebalansi kwa timu zote kupeana zamu ya kumiliki.
Dk ya 46: Taifa Stars wanafika langoni mwa Cape Verde lakini wanakosa umakini.

Timu zinaingia kuanza kwa kipindi cha pili.


Dk ya 44: Cape Verde wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka inakuwa goal kick.
Dk ya 42: Mchezo umesimama kwa muda, kipa wa Stars, Aishi Manula anapatibwa matibabu ya mkono.
Dk ya 41: Mpira bado upo kwenye lango la Taifa Stars.
Dk ya 39: Kona inapigwa almanusura iingine, mpira unatoka unakuwa wa kurushwa kwenda kwa Stars.
Dk ya 39: Almanusura Shomari Kapombe ajifunge baada ya kupiga kichwa kinatoka nje, inakuwa kona.
Dk ya 38: Krosi nzuri ya Samatta inatua kwa Msuva anapiga shuti linatoka nje kidogo ya lango.
Dk ya 35: Mchezo umesimama kwa muda, mchezaji wa Stars yupo chini akipatiwa matibabu.
Dk ya 31: Mashabiki wa Tanzania wanaongeza kasi ya kushangilia.
Dk ya 29: Kazi nzuri ya Samatta inamfanya Msuva kumalizia kwa kufunga bao safi
Dk ya 29: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 27: Tanzania wanaendelea kujipanga taratibu.
Dk ya 26: Cape verde wanapata kona, inapigwa inaokolewa.
Dk ya 24: Timu zinaanza kupeana zamu kumiliki mpira.
Dk ya 22: Mbwana Samatta anakosa penati, mpira unagonga nguzo ya juu na kurejea uwanjani kisha walinzi wanaokoa.
Dk ya 21: Penatiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Tanzania wanapata penati, Msuva anachezewa faulo ndani ya eneo la 18.
Dk ya 20: Garry Rodrigues anapata kadi ya njani kwa kuonyesha nidhamu mbovu.
Dk ya 16: Cape Verde wanafanya shambulizi kali, shuti linapita karibu na lango.
Dk ya 15: Shambulizi lingine, Stars wanashindwa kujipanga vizuri.
Dk ya 13: Stars wanafanya shambulizi, Msuva anapata nafasi anapiga shuti linapaa juu ya lango.
Dk ya 10: Cape Verde wanapata kona, inapigwa inatoka nje inakuwa goal kick.
Dk ya 9: Tanzania wanajaribu kufanya shambulizi la kushtukiza lakini kasi ya Simon Msuva inakuwa ndogo.
Dk ya 6: Wageni Cape Verde wanapiga pasi kadhaa, nao wanaonyesha hawana kasi.
Dk ya 4: Taifa Stars bado wanapanga mashambulizi taratibu.
Dk ya 1: Kasi ya mchezo ni ndogo.
Mchezo umeshaanza
Huu ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2019, mchezo unapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

  1. Mie naamini vijana chipukizi wa Serengeti boys wangefanya kazi nzuri zaidi ya hawa wazee ambao miaka nenda rudi hawana jipya zaidi ya kujiona ni mastaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uxijidsnganye game km LA Leo ujaze madogo wanakula 12-0 sahau kbxa hao ni was kuingiza DKK za nyongeza taratibu wanapata uzoefu

      Delete
  2. Natamani sana Siku moja TFA waweke game kati ya Serengeti boys na Taifa Stars tuone kama wakubwa ndimi hazitawatoka nje nje tumechoka na hiyo Stars isiyofika kokote miaka yote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic