October 17, 2018



SADIO Mane alilazimika kupelekwa hospitalini juzi jioni baada ya kupata majeraha ya mkono. 

Hili ni pigo jingine kwa Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp baada ya awali Mohamed Salah kurejea klabuni hapo akitokea kwenye timu yake ya taifa kutokana na majeraha ya misuli aliyoyapata wakati akiitumikia Misri. 


Mane alipata majeraha hayo kuelekea mechi ya Senegal dhidi ya Sudan, na alionekana akiwa amevaa bandeji katika mkono wake wa kushoto, lakini aliweza kutoa tabasamu mbele ya kamera. 


Hili pia limekuja baada ya beki Virgil van Dijk kurudishwa nyumbani kutokana na tatizo lake lilelile la mbavu ambalo lilisababisha atolewe uwanjani katika ushindi wa mwezi uliopita dhidi ya Southampton. 


Kumbuka pia kiungo James Milner, ambaye msimu huu amekuwa kwenye ubora wa juu, alitolewa nje kutokana na tatizo la nyama za paja katika sare dhidi ya Manchester City kabla ya mapumziko ya kimataifa. 


Liverpool itaitembelea Huddersfield Jumamosi jioni ikitarajia kurudi katika mwendo wa ushindi baada ya kutoa sare kwenye michezo miwili mfululizo ya Premier dhidi ya Chelsea na City.
Majeraha ya Mane na Salah yanaweza yakawapa nafasi Xherdan Shaqiri na Daniel Sturridge wakati kikosi cha Klopp kitakapokwenda kwenye Uwanja wa John Smith Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic