October 17, 2018



Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa ambaye alijiweka kando kutokana na sababu za kiafya huku nafasi yake kukaimiwa na Omary Kaya ambaye anaikaimu amesema kuwa ataweza kurejea Yanga baada ya muda aliojiwekea kupita.

Mkwasa ambaye alifanyiwa upasuaji wa moyo mwanzoni mwa Agosti,mwaka huu anatarajiwa kurejea tena nchini India Novemba 6 mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo huku akisema kuwa anaendelea vizuri.


"Hali yangu imezidi kuimarika kwani nazingatia masharti yote niliyopewa na dokta, pia nahudhuria kliniki kwa dokta Lwakatare, natarajia kwenda India tena kufanyiwa chek up katika hospitali ile ya mwanzo.

"Kuhusu kurejea Yanga nitaangalia baada ya ya miezi sita kupita ndipo nitaamua, kwa sasa nimewekeza nguvu yangu kwenye afya, " alisema.

Mkwasa amewahi kuinoa Yanga kwa nyakati tofauti akiwa kocha msaidizi na wakati mwingine kocha mkuu.

Pia, amewahi kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa Yanga ambao wameweka rekodi kadhaa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic