October 16, 2018


 

Taifa Stars imefuta machungu ya Watanzania kwa kuichapa Cape Verde kwa mabao 2-0 katika mechi ya kuwania kufuzu Afcon kwenye Uwanja wa Taifa.

Kabla, mechi iliyopita Stars ilikubali kipigo cha mabao 3-0 ikiwa ugenini mjini Praia, lakini leo imelipiza kisasi.

Ingeweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, lakini mkwaju wa penalti wa nahodha Mbwana Samatta, uligonga mwamba na kurejea uwanjani kabla ya kuokolewa.


Baadaye, Samatta pamoja na kukosa mkwaju huo aligeuka shujaa wa mechi hiyo baada ya kutengeneza bao la kwanza akimpa pasi safi Saimon Msuva aliyeandika bao la kwanza kabla ya yeye kushindilia msumari wa mwisho akipokea pasi ya kimo cha nyoka ya Mudathir Yahya.









7 COMMENTS:

  1. Ndiyo salehe Jembe na George wenu mjue time nyingi duniani zikicheza nyumbani hufanya vizuri..Sasa kuna timu hapa Tanzania tangu ligi ianze inacheza nyumbani tu!Halafu Saleh Jembe mnaandika eti timu hiyo hivi sasa inafanya vizuri kuzifi Azam na Simba.KUCHEZEA NYUMBANI KUNASAIDIA!Saleh Jembe na wa historia wajue hilo

    ReplyDelete
    Replies
    1. mijitu mingine ka mi bwabwa!!!!!!.......hapa inaongelewa timu ya taifa wao wanaleta mambo ya vilabu.....pumbavu sana

      Delete
  2. Ameshapata majibu huyo wala usihangaike nae hapo ndio wataelewa kwamba mziki wanao pale watakapo anza mechi za ugenini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jana si ulikuwa unashangilia Cape Verde,haya sasa ondoka nao sisi tunabaki na Tanzania yetu.Hongera Stars kwa ushindi murua,wasiopenda soka wajinyonge

      Delete
  3. Ameshapata majibu huyo wala usihangaike nae hapo ndio wataelewa kwamba mziki wanao pale watakapo anza mechi za ugenini.

    ReplyDelete
  4. Ninyi mliotoa comments mbona hamueleweki? Mnazungumzia timu ya taifa au ligi ya vilabu bongo? Yanga na simba zikienda mikoani bado zimamashabiki wengi

    ReplyDelete
  5. Hongera stars ila vita bado mbichi. Lazima tujiulize kwanini tunashindwa kufanya vizuri mechi za ugenini? Mganda kampiga mkepe Verde kwao akarejea tena kumpiga Mlesotho kwao. Kama wachezaji wa stars na Tanzania kwa ujumla tunataka kwenda Cameroon basi piga ua lazima tukampige Lesotho kwao kwani nnaimani Lesotho hatapona kwa mkepe Verde nyumbni kwao hivyo itamfanya cape Verde kuwa na point 7 mbili zaidi yetu. Kupigwa na Mganda kwao haimainishi kuwa Lethoso ni timu dhaifu hapana lazima tuanze kujipanga sasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic