October 22, 2018


TAYARI Taifa Stars imeanza kupewa motisha kuelekea mchezo ujao wa kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho ambao utachezwa ugenini, kisha baadaye dhidi ya Uganda. 

Tumeona Ijumaa iliyopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli akitoa shilingi milioni 50 ili ziweze kusaidia maandalizi ya timu hiyo. 

Pia alitoa wosia kwa wachezaji wa kikosi hicho. Amewataka kufanya kweli kuhakikisha Tanzania inashiriki Afcon mwakani nchini Cameroon. 

Kitendo hicho kilichofanywa na Rais Magufuli ni kizuri na wachezaji wanatakiwa kukichukulia kama sehemu ya heshima kwao na deni ambalo wanatakiwa kulilipa. 


Lakini kuna kitu ambacho mara kadhaa kimekuwa kikijitokeza na huwa kinazifelisha timu nyingi za hapa nyumbani ikiwemo timu ya taifa, Taifa Stars pindi zinapokuwa zinakabiliwa na mechi fulani za kimataifa. 

Hivi karibuni wakati Taifa Stars ilipokuwa ikijiandaa kucheza na Cape Verde mechi ya kwanza, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama halikuonyesha kujali sana, timu ilikuwa kambini, lakini wakati huohuo wachezaji wakawa wanatoka na kwenda kucheza mechi za ligi, kisha wanarudi kambini. Matokeo yake tukafungwa 3-0.

 Makosa kama haya hayapaswi kujirudia tena wakati huu ambao tunazisaka pointi sita kwa udi na uvumba. TFF iipe muda zaidi Taifa Stars wa kujiandaa pindi mechi hizo zinapokaribia. Ikiwezekana hata kusimamisha ligi. 

Tunaamini kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa timu kufanikiwa, lakini ikienda kinyume na hapo, itasaidia kwa kiasi kukubwa timu kufeli.

1 COMMENTS:

  1. Kuelekea mechi ya Lethoso Taifa stars ipo haja ya kuweka kambi fupi ya maandalizi South Africa kulingana na uzito wa mchezo wenyewe hakuna cha kudharau hata kama ratiba ya ligi itapanguka, kwani tumeshasheherekea ligi yetu mara ngapi? mara nyingi tu nani anatuelewa. Shida yetu ni Afcon tukawatangaze akina Samata wengine ,iwe south Africa kwenyewe au hata zambia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic