October 17, 2018





Dalili kwamba Simba imeanza kuvutiwa tena na kiungo wake wa zamani, Ibrahim Ajibu, imewashitua Yanga.


Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, Uongozi wa Yanga umeanza kujifikiria kuhusiana na Ajibu.


“Unajua Simba wameanza kuwapa Yanga presha kuhusiana na Ajibu, maana ni kama wameanza kuvutiwa hivi.


“Uongozi wa Yanga unaliona hilo, tatizo hapa ni suala la fedha za kutosha lakini uongozi unaweza kujipanga.


“Tayari Ajibu amekuwa mchezaji muhimu katika suala la kuiongoza timu maana asipofunga, atatengeneneza nafasi,” kilieleza chanzo.

“Juhudi zinafanyika kwa siri sana ili kuhakikisha fedha zinapatikana na Ajibu anabaki Yanga.”

Hivi karibuni, Ajibu amebadilika na kuwa moto wa kuotea mbali kwani pamoja na kutoa pasi murua za mabao amekuwa akifunga mabao yanayoacha gumzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic