December 15, 2018


Nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa, wana kazi kubwa ya kufanya ili kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Nkana FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika lakini lazima washinde.

Simba itacheza na Nkana ukiwa ni mchezo wa kwanza utakaochezwa nchini Zambia wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ambayo iliondoka Juma­tano ya wiki hii kwenda kucheza mchezo huo, inaisaka nafasi ya kutinga makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya mbele ya Nkana ili tuweze kuvuka hatua hii ambayo kila mmoja wetu hapa anata­mani kuona tunatinga makundi.

“Suala la kwanza hapa ni kushinda na si kitu kingine, hatufikirii matokeo men­gine tofauti, tunataka kufikia malengo yetu na ndiyo maana tunahitaji kushin­da,” alisema Bocco.

Ikumbukwe kuwa, baada ya mchezo huo, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Desemba 23, mwaka huu jijini Dar ambapo mshindi wa jumla atacheza hatua ya Makundi. Atakaye­fungwa, ataenda kucheza mechi za mtoano kuwania kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

5 COMMENTS:

  1. Komaaeni hatuna timu ya taifa zaidi ya simba tuna wategemeeni ili kuiwakirisha Tanzania yetu vizuri

    ReplyDelete
  2. Mungu ni mkubwa atakuwa pamoja nanyi kwa uwezo wake

    ReplyDelete
  3. Naamin MUNGU atatusaidia timu yetu ya simba kushinda

    ReplyDelete
  4. Kila LA heri SSC, naamini mtatutoa kimasomaso, tutawatoa tu hao jamaa pamoja na kuwa walishatutoa awamu 2 kwa ziada ya goli 1. Awamu hii ni wetu mungu awape moyo na ujasiri wa kupambana ugenini na kupata ushindi au walau droo ili mechi ya 2 tuwachinjie pale taifa. Jamaa inaonesha huwa wanategemea sana uwanja wao kwani ugenini hawana chochote. So in kuwamaliza mapema hukohuko kwao. Aminia sana SSC, Kila LA kheri.

    ReplyDelete
  5. Kila la kheri timu yetu ya simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic