December 15, 2018


Kampeni za wagombea wa nafasi mbalim­bali za uongozi ka­tika Klabu ya Yanga zilizopangwa kuanza juzi Alhamisi, zimea­hirishwa baada ya wagombea kuhofia usalama wao.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imalize kuwafanyia usaili katika kuelekea uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Januari 13, mwaka huu.

Wagombea hao waliopitishwa na TFF wamekumbana na ugumu kutoka kwa wanachama wa Klabu ya Yanga ambao wanawatuhumu kuwa ni wasaliti baada ya kukubali uchaguzi wao usimamiwe na shirikisho hilo.

Jumatatu ya wiki hii katika kikao cha viongozi wa Kata Tano za Matawi ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kilichofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo Jangwani, Dar yalitolewa mapendekezo kwa wagombea hao wote kufutwa uanachama baada ya kukiuka katiba ya Klabu ya Yanga.

Kikao kiliongozwa na mwenyekiti wa Kanda ya Dar, Shabani Uda ambaye pia ni Katibu wa Tawi la Manzese ambaye alisikika akisema: “Hatutakwenda kupiga kura siku ya uchaguzi kama TFF waking’ang’ani kuendelea kutusimamia uchaguzi wetu.”

“Ikumbukwe kuwa tangu TFF ilipotangaza kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa Yanga bila kuwahusishwa viongozi wa timu hiyo, tahadhari ilitolewa juu ya uwezekano wa mchakato huo kukamilika kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wanachama wa klabu kupitia katiba yao.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic