December 15, 2018


TUHUMA ZA UBADHIRIFU

Tayari suala hili tumelitolea ufafanuzi licha ya baadhi yao kuendelea kulizungumza lakini ukweli ni kwamba kinachozungumziwa kimejikita kwenye Taarifa ya Hesabu za TFF za mwaka 2015 na 2016 zilizopokelewa tarehe 11 Septemba 2016 na tarehe 27 Novemba 2017 kwa mfuatano na kufanyiwa kazi.

Katika kipindi hicho kilichotajwa kimekuwa chini ya ukaguzi wa PCCB na tayari mashauri yako mahakamani yanaendelea ikiwa ni pamoja na kufuatilia waliotajwa katika hesabu za fedha katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016.

Kwa kuwa masuala hayo yapo kwenye ngazi ya mahakama, TFF inaona  iviachie vyombo vya kisheria vifanye kazi yake kadiri ya taratibu zao.

Kitu ambacho hakipo sawa ni kuhusisha uongozi uliopo madarakani chini ya Rais wake Ndugu Wallace Karia ambapo wakati wa tuhuma hizo uongozi huu ulikuwa haujaingia madarakani.

SUALA LA FEDHA ZA MTIBWA SUGAR (ASFC)

Suala hili limekuwa likipotoshwa na kupindisha ukweli wa jambo hili.

Bado suala la fedha za zawadi halijakamilika mpaka sasa hatujapokea fedha ya zawadi tupo kwenye mchakato wa kupokea fedha hiyo ya zawadi kutoka Azam Tv.

MUUNDO WA TFF NA VYOMBO VYAKE 

Mkutano mkuu ndiyo wenye maamuzi ikifuatiwa na Kamati ya Utendaji na Kamati zetu ndogondogo zipo huru na haziwezi kuingiliwa na yeyote hata Rais wa TFF hawezi na hajawahi kuziingilia kwahiyo kila maamuzi ya Kamati hizo yapo huru.

Adhabu zote zinazotolewa na Kamati hizo zinatumia Katiba ya TFF ya mwaka 2013 iliyofanyiwa marekebisho 2015.

Kuna watu wamefungiwa na Kamati ya Maadili wanalalamika pembeni pasipo kufuata utaratibu wa kikatiba.

Kesi ya Viongozi wa Arusha waliofungiwa ilitokana na mchezo kati ya Arusha United dhidi ya Simba iliyochezwa Agosti 15,2018 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Katika mchezo huo fomu ya mapato inaonesha TFF imechukua mapato baada ya mchezo huku pia katika makato hayo ikikatwa fedha ya BMT,VAT na gharama ya mchezo fedha ambazo hazikuwasilishwa sehemu husika.

Katika michezo ya kirafiki TFF huwa haichukui mapato inaziachia klabu ziweze kujiongezea kipato lakini kwenye mchezo huo viongozi hao wamechukua fedha ya TFF ambayo tulielekeza isichukuliwe.

SHUGHULI ZA KARIBUNI MAENDELEO 

Shughuli yetu kubwa ni mpira na ndio maana tunahakikisha shughuli za mpira wa miguu zinakwenda.

Timu zetu za Taifa Klabu zimekuwa zikishiriki na kufanikiwa katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki 

Mashindano mbalimbali tuliyoshiriki au kuandaa 

Machi tumecheza mchezo wa Kufuzu AFCON ya Wanawake dhidi ya Zambia ambao walituondoa kwa sheria ya goli la ugenini.

Aprili 2018 Serengeti Boys wamefanikiwa kuwa Mabingwa wa CECAFA huko nchini Burundi.

Mei Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL imechezwa kwa mafanikio makubwa vituo vya Geita, Rukwa, Singida, Kilimanjaro kiasi cha kuwavutia Malawi ambao wanataka kuiga mfumo huo.

Juni Fainali za Azam Sports Federation Cup ASFC ilifanyika Arusha ikiwakutanisha Mtibwa Sugar na Singida United.

Juni 2018 tumecheza Ligi ya U20 Iliyofanyika Dodoma wakati Juni 2018 Kilimanjaro Queens wakawa Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo wa kwa Wanawake Ukanda wa CECAFA Mashindano yakofanyika Rwanda
Julai 2018 Azam FC wakawa Mabingwa CECAFA Kagame Cup mashindano yakifanyika Dar es Salaam 

Agosti 2018 Serengeti Boys ikicheza michezo ya Kufuzu Afcon Ukanda wa CECAFA ikafanikiwa kumaliza na kupata nafasi ya Mshindi wa 3.

Tuna mashindano makubwa mwakani ya U17 AFCON yatakayofanyika hapa Tanzania ambapo droo yake inatarajia kufanyika Disemba 20,2018.

Timu yetu ya Taifa inacheza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu Afcon dhidi ya Uganda mwakani ni mchezo muhimu ambao tukishinda tunaingia AFCON baada ya miaka 38.

Novemba 2018 Tanzania ilifanikiwa kuwa Mabingwa wa mashindano ya Copa Dar Es Salaam katika mchezo wa soka la Ufukweni mashindano ambayo yalihusisha nchi za Uganda,Mauritius,Malawi na Tanzania 

Timu yetu ya Taifa ya U17  Serengeti Boys ipo kwenye mashindano ya COSAFA ambako imefanikiwa kuingia Fainali,mashindano yakifanyika huko Gaborone Botswana.

Simba na Mtibwa Sugar wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa nao wanaendelea kufanya vizuri katika mechi zao wanazocheza jambo ambalo linaonesha namna kiwango cha Tanzania kinavyoendelea kupanda.

Tukumbuke katika Kanda ya CECAFA kwasasa Tanzania ndio tunatawala katika upande wa Soka la Wanawake,Vijana na ngazi ya klabu.

Tanzania ndio mfano wa kuigwa Africa katika Mpira wa Wanawake na uendeshaji wa Ligi Daraja la Kwanza.

Wenzetu wa FC Twenty ya Uholanzi wameonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Shirikisho katika upande wa Mpira wa Wanawake.

Katika matumizi ya fedha za Shirikisho tumekuwa tunajitahidi kupata mechi katika wakati wote wa kalenda ya tarehe za FIFA na aina ya timu ambazo tumeanza kuzipata ni zile zenye ushindani kama tulivyocheza na DR Congo na Algeria.

SEMINA/MAFUNZO 
Semina mbalimbali zimefanyika na zinaendelea kufanyika kwa wadau wetu 

Kozi mbalimbali zinafanyika ikiwemo kozi za soka la Vijana na Wanawake.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na Kocha Mkuu wa timu za Taifa wanaendelea na mafunzo pamoja na zoezi la kutafuta vijana wenye vipaji tayari wamefanya Arusha na kupata vijana 22 na kesho watakua Mwanza kuendelea na zoezi hilo.

Waamuzi wetu wameendelea kuaminiwa na CAF kuchezesha mechi mbalimbali ikiwemo kuchezesha mashindano makubwa ya Africa.

Viongozi tofauti wamekuwa wakiaminiwa kusimamia mashindano au mechi mbalimbali.

TFF tumeamua kuwalipa Wakufunzi ambao wamekuwa wanakuja kutoa mafunzo mbalimbali kwa makocha na Waamuzi.

KESI ZILIZOPO MAHAKAMANI 

Kwakua kesi hizi zipo mahakamani hatuwezi kuzizungumzia kiundani lakini TFF tulichofanya ni kukata rufaa juu ya maamuzi yote ya mahakama kwasababu hatupingani na Mahakama na nia yetu ni kuelezea kiusahihi kuhusu utaratibu na ngazi za kufuata katika masuala yanayohusu Kamati zetu ambazo zipo huru.

Kesi zetu kwa sasa atakua anazisimamia Wakili maarufu Alex Mgongolwa.


RIPOTI YA FEDHA NA RIPOTI YA UKAGUZI WA MAHESABU 

Ripoti ya Ukaguzi wa fedha ni ripoti ya siri ambayo inapaswa kwenda kwa taasisi na sio kwenye umma na ripoti ya fedha ndio ambayo ikishafanyiwa kazi inaweza kuwekwa hadharani.

Ni vyema vyombo vya habari vinapozungumza masuala kama haya vikafanya kwa kufuata taaluma ya eneo husika.

Clifod Mario Ndimbo 
Afisa Habari na Mawasiliano,TFF 

1 COMMENTS:

  1. mnataka ripoti ya fedha ya TFF iwe siri kwani shirikisho ni la baba yenu acheni upuuzi kama mngekuwa wasafi msingefanya siri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic