December 14, 2018




Beki Kelvin Yondani atakaa nje wakati Yanga ikivaa Ruvu Shooting, keshokutwa.

Yondani atalazimika kukaa jukwaani kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Beki huyo na nahodha wa Yanga analazimika kukaa nje ikiwa ni sehemu ya sheria za soka.

Hata hivyo Yondani amekuwa sehemu ya mhimili wa ulinzi wa Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekuwa akisisitiza kuwa na aina ya kuziba mapengo kwa kuwa ni lazima timu itapata misukosuko.

Yanga ambao hawakutarajiwa, wameendelea kuongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 41, wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 40 na Simba 27.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic