December 15, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amekataa kumpokea kipa wake Beno Kakolanya baada ya kugomea kuitumikia timu yake kutokana na madai ya kutolipwa stahiki zake.

Hivi karibuni Kakolanya aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza kulipwa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wa miezi kadhaa ambao hajapata mpaka sasa.

Maamuzi hayo ya Kakolanya kugoma yalifanya Zahera aibuke kupitia vyombo vya habari na kuelezwa kushangazwa naye mpaka imefikia hatua ya kutomhitaji tena katika kikosi chake.

Aidha, Zahera ameongeza kwa kumtaka mchezaji huyo ni vema akatafutiwa timu nyingine kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho saa 6 kamili usiku kwa maana yeye hamhitaji tena.

"beno hawezi tena kurudi kwenye timu, walimwambia asije mazoezini hivyo wanapaswa kumtafutia timu nyingine, ila hapa kwetu nadhani haitawezekana tena" amesema.

Inaelezwa Kakolanya anaidai Yanga kiasi cha shilingi za kitanzania, milioni 15 kama fedha ya usajili pekee ukiachana na zile za mshahara.


4 COMMENTS:

  1. Karibu Msimbazi Kakolanya japo ulitufanyia umafia mechi ya Simba vs Yanga

    ReplyDelete
  2. Mpira ndio unaompa chakula yeye na aila yake, kudai mishahara na haki zake nyengine ni usaliti?

    ReplyDelete
  3. Kudai haki yako ni kosa? Kavumilia vya kutosha. Mshahara na pesa za USAJILI ale nini?

    ReplyDelete
  4. Kocha yuko sahihi timu ikifungwa ndiye anayebeba lawama zote sio mchezaji. Kwa hiyo wote wangegoma kama yeye timu ingeshushwa daraja leo angerudi wapi? Au amesikia Yanga imepata mfadhili? Atagoma tena mbele huko. Kanuni inasema usipolipwa ugome au uvunje mkataba? Hadi sasa Beno ndiye mkosaji kwa kutoroka kazini vinginevyo angevunja mkataba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic