January 20, 2019


BAADA ya kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu Bara jana dhidi ya Mwadui FC, kikosi cha Azam FC kimeweka kando nguvu zao kwenye ligi na kuelekeza kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho.

Azam walishinda bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wao Donald Ngoma dakika ya 70 na kuwafanya wabebe pointi tatu wakiwa Uwanja wa nyumbani Chamazi.

Mchezo wao wa FA watacheza kati ya tarehe 25 au 28 dhidi ya kikosi cha Pamba kutoka Mwanza, Uwanja wa Chamazi.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema wanaimani ya kufanya vizuri katika michezo yao ya FA kwa kuwa malengo yao ni kuona wanabeba pia kombe hilo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic