January 20, 2019


BAADA ya kikosi cha Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda kufungwa bao 5-2  dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili, leo Coastal Union wameibuka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga, ulikuwa na ushindani mkubwa kwani iliwalazimu Coastal Union kusubiri mpaka dakika ya 49 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Andrew Simchimba.

Dakika za lala salama, Coastal Union walifanikiwa kuongeza bao la pili la ushindi ambalo liliwamaliza nguvu African Lyon ya kupata ushindi kutokana na bao hilo lililofungwa na Issa Abushee dakika 90.

katika michezo mingine ya Ligi Kuu Bara leo Ruvu Shooting wametoka suluhu na Tanzania Prisons, Kagera Sugar wameshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic