January 20, 2019


Mwaka 2003 Enyimba ya Nigeria walianza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Simba kwao katika Ligi ya mabingwa Afrika.

Mechi ya pili wakafungwa na Ismailia 6-1 ugenini, wakajipanga katika mechi zinazofuata hatimaye mwaka huo huo wakachukua ubingwa wa Afrika.

Inawezakana kabisa tukapindua matokeo kama Enyimba,muhimu ni kujua tuliteleza wapi na nn tufanye mbele ya safari!!

Hao wanaowacheka leo habari zao kwetu ndio kama mnavyosoma hapo juu.

Waache wacheke leo sisi tutacheke kesho.


4 COMMENTS:

  1. Watu watatushangaa tunavyotaka kucheza nje ya uwanja...watahc tumefeli. Ndio Hadith za Manara zinapokwenda. Tukae tuwaze kwann kocha anashindwa kuwa na mbinu mbadala za uchezaji. Hiki ndio kitu kikubwa. Tusitafute mchawi was mbali. Jana tulipotezwa sana na wala si kitu kingne. Tujipange kwa mtanange wa tarehe 1 mwez ujao pale Misri

    ReplyDelete
  2. Manara hajazungumzia lolote kuhusu mambo ya nje ya uwanja.
    Tumefungwa kama ilivyo kawaida ya matokeo ya mpira.
    Timu hii ya Simba haijapata changamoto za kufungwa bao nyingi labda itawasaidia kujifunza kuheshimu wapinzani wao.
    Kocha lazima acheze soka la kujihami wakiwa ugenini .

    ReplyDelete
  3. Soka ya ushindani kimataifa bado sana Tanzania, wachezaji wetu pamoja na sifa na uwezo tunaojaribu kuwapa bado ni duni ukilinganisha na wenzao kunahitajika mapinduzi makubwa kwani mpira sio tu ni sayansi bali ni biashara kubwa

    ReplyDelete
  4. Wale AS Vita ni level nyingine kabisa.....sio level yetu.Simba wangepigwa hata goli kumi juzi,kuna mambo mawili yaliwaokoa wasipokee aibu kubwa zaidi;(1)Manula aliiokoa sana simba juzi,alicheza ktk kiwango ambacho nilikiona mara ya mwisho akiwa azam,kwangu naweza kusema ndio alikuwa man of the match kwa upande wa simba,(2)As Vita wana mpira wa kasi na pumzi nyingi huku wakitumia counter attack mara nyingi,simba walikuwa wakicheza mpira wa taratibu huku wakipiga pasi nyingi.mbinu ile iliwaokoa sana kwani ilikuwa inapunguza uchu wa magoli wa As Vita,lakini simba wangejichanganywa nao wakacheza mpira wa kasi wangewapa mwanywa Vita kuwapiga bao nyingi wakitegemea silaha yao ya kasi na pumzi kwakuwa simba wangekuwa wanakwenda kushambulia na wangezidiwa kwa pumzi na kazi endapo kibao cha kushambulia kingegeukia kwao ghafla.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic