January 20, 2019


WAWAKILISHI pekee wa Afrika Mashariki kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana usiku mbele ya AS Vita walikiona cha moto jijini hapa.

Walikumbana na kipigo cha mabao 5-0 na kujikuta wakiporomoka hadi nafasi ya tatu kwenye kundi lake linaloongozwa na Al Ahly ya Misri yenye pointi nne.

Katika michezo 21 ya Ligi ya Mabingwa Afrika waliyocheza nyumbani mjini hapa, AS Vital ilipoteza mmoja tu. Imeshinda 16 ukijumuisha na ule wa jana dhidi ya Simba na sare tano.

Mchezo huo ulikuwa mgumu huku Simba wakionekana kuwa na wakati mgumu licha ya kuanzisha muziki wake wote. 

Tathmini ya kiufundi kwenye mchezo huo ilionyesha kwamba Simba ilizidiwa idara zote na Vita walitumia uzoefu wao kumaliza mchezo huo mapema.

Vita walionyesha ukomavu wao kwenye michuano hiyo kwa kujiamini na kutulia muda mwingi wa mchezo huo.

Simba ambao waliambatana na viongozi wao wakubwa jijini hapa walijitahidi kutulia na kurudi mchezoni lakini mastaa wao wengi akiwemo Claytous Chama, Emmanuel Okwi walionekana kufichwa.

Kikosi cha Simba kilichoanza kilikuwa na Aishi Manula, Nicholas Gyan, Tshabalala, Juuko Murshid,Wawa,Kotei,Mzam iru,Mkude,Kagere, Okwi na Chama.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Simba ilikuwa imefungwa mabao matatu na cha pili wakaongezwa mawili. Mechi ijayo Simba itacheza na Al Ahly nchini Misri Februari 2.

1 COMMENTS:

  1. Sasa hapo kimevuja nn? Waandishi MNA matatizo sana... Eti Imevuja..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic