January 20, 2019



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo amesema kilichowaponza Simba kufungwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita ya Congo ni kutoupa uzito mkubwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zahera ambaye kabla ya mchezo aliwashauri Simba kutowaruhusu wapinzani wao kuwa na umiliki wa mpira muda mwingi kutokana na spidi ya wachezaji wa AS Vita na kuwasihi washambuliaji wa timu hiyo kutafuta bao la mapema dakika tisini mambo yakawa tofauti.

"Nimewaangalia wachezaji wa Simba namna ambavyo walikuwa wakicheza, nimeumia sana kwa kuwa wamenishangaza namna ambavyo walikuwa wakiyachukulia mashindano ya Ligi ya Mabigwa kama mchezo wa kirafiki wakati ni mashindano makubwa.

"Utaona baada ya kufungwa wachezaji walikuwa wakisimama na kuishia kujishika mikono kiunoni, morali yao ilikuwa chini hali iliyowafanya washindwe kupata matokeo, wanapaswa wabadilike na wasichukulie wepesi michuano hii kwani wana timu nzuri, wacheze wakiwa ni timu na sio mchezaji mmoja," alisema Zahera.

Kwa matokeo hayo waliyoyapata Simba wanashushwa nafasi ya kwanza waliyokuwa na kushika nafasi ya tatu huku kinara akiwa ni Al Ahly mwenye pointi nne kwenye kundi D.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic