January 20, 2019



NYOTA wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka, ameibuka Mfungaji Bora (Best Scorer) wa Ligi ya Kikapu kwa Taasisi za Fedha (Bankers Basketball League BBL 2018/19), baada ya kufunga pointi 160 katika mechi za michuano hiyo iliyofikia tamati jana, jijini Dar es Salaam.

Fainali ya kukata na shoka ilifanyika jana Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, Benki ya DTB iliibuka mshindi baada ya kuifunga NMB kwa pointi 90-73, huku Leka akifunga zaidi ya nusu ya pointi zao na kutangazwa mfungaji bora akifuatiwa na Acram Majid wa DTB, aliyefunga pointi 129.



Leka alizawadiwa tuzo ya mfungaji bora, Mchezaji Bora alikuwa (MVP) Leonard Benedict wa DTB, Beki Bora Frank Mwemezi wa DTB na kinara wa kufunga pointi tatu kwa mtupo mmoja (Leading Three Pointer), Acram Majid aliyefanya hivyo mara 13 katika michuano yote.

Mratibu wa BBL 2018/19, Gozbert Boniface, alizipongeza timu sita zilizoshiriki michuano hiyo kwa upande wa mpira wa kikapu na kuzitaka kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao, utakaoanza baadaye mwaka huu.

“Tunaipongeza DTB kwa kutwaa taji, lakini pia kwa NMB kwa kutwaa medali za fedha za ushindi wa pili na pia kwa kutoa Mfungaji Bora wa michuano hii, iliyoshirikisha benki sita ikiwa ni pamoja na NMB, DTB, Azania, CRDB, TADB na NBC,” alisema Boniface.

Mgeni Rasmi wa fainali hiyo, Juma Kimori, ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, aliwapongeza waratibu kwa wazo zuri la kuanzisha michuano hiyo, iliyoimarisha mahusiano baina ya taasisi za kifedha nchini, huku akiwapongeza mabingwa na washindi wa pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic