January 11, 2019


MCHEZO wa nusu fainali ya pili kati ya Simba na Malindi kwa sasa ni dakika 90 zinakamilika hakuna aliyena lango la mwenzake katika Uwanja wa Amaan.

Timu zote zimecheza kwa kushambuliana na mpira wa pasi za chini hali inayofanya kuwe na burudani safi kwa mashabiki leo.

Viungo wa timu zote mbili wamecheza kwa kujituma na kuonesha udambwiudambwi Uwanjani, Malindi wanashambulia kwa kushtukiza huku Simba wakiwategemea zaidi viungo wao wakiongozwa na Mohamed Ibrahi 'Mo'

Simba wamefanikiwa kupata kona nne Uwanjani ambazo zote hazijazaa matunda huku Malindi wakiwa wamepata kona moja.

Kwa matokeo hayo mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti ili kumfuata Azam Januari 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic