January 20, 2019


UONGOZI wa Azam FC umesema umewapa kazi nyingine washambuliaji wao wa kimataifa, Donald Ngoma na Obrey Chirwa wanapaswa waikamilishe ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema baada ya washambuliaji hao kukamilisha kazi ya kwanza bado wana kazi nyingine kubwa za kufanya kwa ajili ya klabu yao.

"Lengo la kwanza ilikuwa ni kubeba kombe la Mapinduzi tuliwaambia wafanye jitihada zao kwa kushirikiana na wachezaji wote wa timu wamefanikiwa sasa kazi mpya inakuja ni kubeba makombe mawili yaliyobaki.

"Tunashiriki michuano ya kombe la Shirikisho 'FA' na Ligi Kuu Bara tunahitaji kuyabeba haya makombe hivyo kazi yao nyingine iliyobaki ni kuona tunaweza kubeba haya makombe pia," alisema Alando.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic